
JUAN
Mata amewaomba radhi mashabiki wa Manchester United kwa kiwango kibovu
kwenye mchezo wao dhidi ya Leicester City na kusema anashiriki nao
katika maumivu waliyoyapata baada kushindwa kuulinda uongozi wao wa
mabao mawili.
United
iliongoza 2-0 na baadae 3-2 kwenye uwanja wa King Power lakini
ikajikuta ikichukua kichapo cha 5-3 katika mchezo ambao nyota huyo wa
Hispania anauelezea kuwa ulikuwa wa kukatisha tamaa.
Mata
amewaahidi mashabiki wao kuwa United itarejea na nguvu mpya katika
mechi zao mbili zijazo za uwanja wa nyumbani dhidi ya West Ham na
Everton.
Akiandika
kwenye blog yake, Mata ambaye aliingia badala ya Angel di Maria dakika
14 kabla mpira haujaisha, alisema baada ya kusubiri mechi kwa wiki
nzima, kamwe hakutegemea kukumbana Jumapili ya aina hiyo.
No comments:
Post a Comment